Subscribe | NSW Fair Trading | Glossary | Contact us | Search
Email link to this page Print this page Reduce font size Increase font size

Uwakilishi - Representation

 More information in Swahili

Upande wa utendaji wa CTTT ushauriliwa kuendesha kesi yao yenyewe bila uwakilishi wa kisheria – section 36(1) Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Act 2001. Hii inaruhusu CTTT kutoa njia za kupatikana na za kufaa kutatua mabishano.

Hata hivyo, CTTT inaweza kukubali uwakilishi wa kisheria katika hali fulani inavyoelekezwa na Part 4 Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Regulation 2009.

Kuwalikisha mwenyewe

Pale CTTT, utashauriliwa kuendesha kesi yako yenyewe bila uwakilishi. Ingawa kujiwakilishi inaweza kuonekana kuwa kazi ya kuogofya, waweza kutazamia jambo lako litasikilizwa na kuamuliwa sawa na kulingana na sheria.

Kuwalikisha mwenyewe pia kuna faida ya kukupa amri ya kweli juu ya jinsi kesi yako inavyotambulishwa kwa CTTT. Ukiandaa na kupanga vizuri, waweza kuwa mtetesi mwenyewe wako mzuri sana katika hukumu.

Getting help fact sheet (PDF size: 341kb) (Karatasi ya hakika ya Kupata msaada, Kupatikana kwa Kiingereza tu) inaorodhesha huduma anuwai kubwa katika NSW zinazoweza kukusaidia na maswali ya kisheria.

Maombi kupata mwakilishi

Katika hali fulani CTTT inaweza kuwaza kuruhusu uwakilishi. Unaweza kuomba kuwakilishwa kutumia maandishi au unaweza kuomba wakati wa hukumu. Mjumbe wa Baraza ataamua siku ile kama unaweza kuwakilishwa.

Kuomba kwamba uwakilishwe katika utendaji, ombi lifanywe katika maandishi na kuwa maelezo yafuatayo ndani:

  • Nambari ya faili na majina ya watu/upande
  • Sababu kwa nini ni kutafuta ya kuwakilishwa
  • Jina na kazi ya mwakilishi ambaye anapendekezwa na kwa vyovyote mtu yule ni mwanasheria
  • Taarifa kwamba mwakilishi anayependekezwa ana ruhusa yako kufanya maamuzi wakati huyupo ambayo lazima kufuatwa.

Sababu za uwakilishi

CTTT anaweza kuamua kuruhusu uwakilishi katika hali ifuatayo– clause 14 Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Regulation 2009.

Mwakilishi wako anaweza kuwa mwanasheria, ajenti wa mali isiyohamishika kwa niaba ya mwenye nyumba, mtetesi, rafiki au ndugu/jamaa kwa sharti umempa mamlaka kutenda kwa ajili yako na kumruhusu kufanya uamuzi kwa niaba yako katika hukumu.

Uwakilishi wa kisheria

Waweza kuomba kuwakilishwa kwa maandishi kabla kesi hajasikilizwa au waweza kuomba wakati wa hukumu ya kwanza. Ukifanya ombi lako kwa kutumia maandishi, CTTT atatafuta maoni kutoka upande mwingine kabla ya kuamua uamuzi.

Kama Mjumbe wa Baraza anaamua unaweza kuwakilishwa, upande mwingine ataweza pia kuwakilishwa.

Uwakilishi mwingine

Waweza kuomba ruhusa kuwakilishwa katika hali moja au zaidi ifuatayo:

  • Katika mambo ya Idara ya Kujenga Nyumba kuhusisha dai au bishano kwa kiasi juu ya $30,000
  • Ambapo chama wa mashitaka ni:
    • Mwenye nyumba kuwakilishwa na ajenti wa kusimamisha mali
    • Mwenye kiwanja cha makazi kuwakilishwa na meneja wa kiwanja
    • Mwendeshaji wa kijiji cha kustaafu kuwakilishwa na mfanyakazi au ajenti
    • Mkazi wa kijiji cha kustaafu kuwakilishwa na mkazi aliyependekezwa wa kamati wa kijiji au wakazi
    • Shirika kuwakilishwa na mmojawapo wa maafisa yao
    • Shirika la wamiliki (tabaka) kuwakilishwa na ajenti wa kusimamisha tabaka
    • Chama cha jamii kuwakilishwa na mmojawapo wa wajumbe wake au ajenti wa kuongoza
    • Chama cha ushirika kilichosajiliwa kuwakilishwa na mmojawapo wa maafisa yake
    • Washirika kuwakilishwa na mmojawapo wa mbia wake
    • Chama kilicho shirikishwa kuwakilishwa na mmojawapo wa maafisa yake
    • Chama kisichoshirikishwa kuwakilishwa na mjumbe aliyechaguliwa wa kamati ya utendaji au ya kuongoza
    • Mali inayosimamishwa na mdhamini
    • Shirika la serikali kuwakilishwa na afisa
  • Kama upande mwingine utawakilishwa na mwanasheria
  • Kama upande mwingine ni shirika la serikali
  • Kama CTTT anaona kwamba masuala magumu ya kisheria au hakika yatatokea katika utendaji.

Mambo ya mipango ya tabaka na jamii

Upande kuhusisha mabishano ya mpango wa tabaka au mpango wa jamii unapewa uwakilishi mara moja, na hakuna haja kuomba ruhusa ya CTTT.

Section 193 ya Strata Schemes Management Act 1996 inaeleza kwamba upande katika jambo la mpango wa tabaka unaweza kuwakilishwa mbele ya CTTT.  Section 93 ya Community Lands Management Act 1989 inaruhusu sawa kwa mambo ya mipango ya jamii.

Watu wenye hali ngumu

Kama Mjumbe wa Baraza anagundua upande mmoja ni mwenye hali ngumu au hana uwezo wa kutosha kuendesha kesi yake, anaweza kuamua amri kuelekeza wawakilishwe – section 36(6) Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Act 2001.

Chini ya Sheria, watu wana hali ngumu kama ni watoto wenye umri chini ya kumi na nane au watu ambao hawawezi kujiwakilisha kwa sababu ya ulemavu wa akili, kimwili, kisaikologi au ya fahamu, umri kubwa sana, ukosefu wa akili au ulemavu mwingine.

Wakalimani

CTTT inatoa huduma ya mkalimani bila malipo kwa hukumu. Ukihitaji mkalimani, wasiliana na CTTT kwa nambari 1300 135 399 mara moja ili mipango inaweza kupangiliwa. Familia/ndugu au marafiki hawaruhusi kutafsiri katika utendaji wa CTTT.

Mjumbe wa Baraza anaweza pia kuomba mkalimani akiona mtu hawezi kuelewa utendaji wa kutosha.

Top of page

Other topics available in Swahili:

•  Njia ya upatanisho - Conciliation process
•  Kuandaa upatanisho - Preparing for conciliation
•  Kutayarisha kwa hukumu - Preparing for hearing (PDF size: 357kb)
•  Maamuzi na amri - Decisions and orders
•  Kurudia hukumu na kukata rufaa - Rehearing and appeals (PDF size: 354kb)
•  Tunachoweza na hatuwezi kufanya - What we can and cannot do (PDF size: 356kb)

Get a free copy of Adobe Acrobat Reader so you can access PDF versions of our information.


Email link to this page Print this page Reduce font size Increase font size