Subscribe | NSW Fair Trading | Glossary | Contact us | Search
Email link to this page Print this page Reduce font size Increase font size

Information on this topic also available for:

Kuandaa upatanisho - Preparing for conciliation

More information in Swahili

Kuwa tayari na wazi kuhusu matokeo unayotaka ni njia nzuri sana kujitayarisha kupatanisha. Hii ni muhimu bila kujali kwa vyovyote kama wewe ni mwombaji au mshtakiwa.

Mashauri kumi juu ifuatayo yanaweza kukusaidia kuandaa na kupata faida zaidi kutoka njia ya upatanisho.

Mashauri kumi juu ya upatanisho

1. Fikiria kuhusu unachotaka

Fikiria kwa uangalifu kuhusu masuala yako na matokeo unayotaka kufaulu. Andika muhtasari ya masuala haya.

2. Panga jinsi unatakavyokubaliana

Uwe tayari kupokea mawazo na kubadilisha. Fikiria kuhusu masuala ya mtu mwingine na jinsi atakavyopokea maoni yako. Kupatana kunaweza kuhusisha kila upande kulegeza madai yake ili kufikia maafikiano ambayo yanafaa kwa nyote wawili.

3. Sema upande wako wa maelezo

Eleza kwa ufupi upande wako wa maelezo na onyesha ushahidi wako kwa mtu mwingine. Eleza jinsi unavyotaka kutatua mabishano. Lenga utatuzi. Jaribu kutobishana kuhusu nani ni sahihi au si sahihi, au maana.

4. Sikiliza mtu mwingine

Sikiliza kwa uangalifu mtu mwingine na angalia ushahidi wao. Labda utataka kuandika vidokezo. Umpe nafasi kuongea na usiingilie. Jaribu kufikiri maoni yao, hata usipoyakubali.

5. Lenga masuala, na sio hisia

Endelea kulenga masuala, na sio hisia au matendo ya mtu mwingine.

6. Anza kujadiliana

Anza kuwaza utatuzi unaowezakana. Fanya fadhila na fadhila ya kujibu fadhila. Upatanisho wa mafanikio unatokea wakati upande wote wawili wanapokubali utatuzi.

7. Kubali tu kwa mambo unayoona yanafaa

Uwe na hakika unakubali kwa matokeo pekee unayoona yanafaa. Kumbuka kwamba lazima kuwa na maafikiano katika kufika mapatano.

8. Omba kwa msaada kama una matatizo

Kama una matatizo, omba Mwamuzi, Mjumbe wa Baraza au Afisa wa Usajili kwa msaada. Kama ukijisikia kutishwa na mtu mwingine yule, umwambie Mwamuzi au afisa wa ulinzi mara moja.

9. Ukifika mapatano

Andika mapatano yako kwa fomu inayotolewa. Kama Mwamuzi amepatikana anaweza kukusaidia kuyaandika. Kabla mapatano yako kuwa amri ya kisheria ya lazima kufuatwa, utaulizwa kama unaelewa mapatano, na kuhakikisha umekubali kwa hiari.

10. Usipofika mapatano

Usipofika mapatano, hukumu itaendelea siku ile au tarehe ya baadaye. Fikiria kama masuala yako ni muhimu ya kutosha kurudi siku nyingine inavyoweza kuzidisha muda, gharama na usumbufu kwako.

Top of page

Other topics available in Swahili:

•  Njia ya upatanisho - Conciliation process
•  Kutayarisha kwa hukumu - Preparing for hearing (PDF size: 357kb)
•  Uwakilishi - Representation
•  Maamuzi na amri - Decisions and orders
•  Kurudia hukumu na kukata rufaa - Rehearing and appeals (PDF size: 354kb)
•  Tunachoweza na hatuwezi kufanya - What we can and cannot do (PDF size: 356kb)

Get a free copy of Adobe Acrobat Reader so you can access PDF versions of our information.


Email link to this page Print this page Reduce font size Increase font size