Information on this topic also available for:
Maamuzi na amri - Decisions and orders
| More information in Swahili |
Baada ya Mjumbe wa Baraza ameamua amri, upande wote wawili wapokee nakala ya kuchapishwa ya amri ndani ya siku 7 baada ya hukumu. Kama Mjumbe wa Baraza anaahirisha uamuzi, ndipo amri na sababu za maandishi kwa uamuzi itapelekwa tarehe ya baadaye.
Aina ya amri
Aina ya amri ambayo CTTT inaweza kuamua inategemea Idara iliyopo ombi iliwekwa. Angalia application form (Kupatikana kwa Kiingereza tu) kwa kila Idara kuona orodha ya aina ya amri inayoweza kuamuliwa.
Amri nyingi yao ya CTTT inagawa kwa vikundi viwili:
- Amri kwa mtu au kampuni akulipe fedha
- Amri kwa mtu au kampuni amalize kazi fulani.
Aina nyingine ya amri inayoweza kuamuliwa ni pamoja na:
- Amri kwamba huna deni ya fedha kwa mtu au kampuni
- Amri kubadilisha kitu kibaya
- Amri kwa ongezo ya kodi inayopendekezwa ni kubwa mno.
Gharama
Kawaida kila upande ulipe gharama zao zenyewe. CTTT inaweza kuamua gharama kulipiwa katika hali fulani, kama ombi linaonekana ni la kipuuzi, chushi, kuelewa vibaya au kukosa nguvu, au upande una wakilishi wa kisheria.
Angalia clause 20 (Kupatikana kwa Kiingereza tu) ya Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Regulation 2009 kwa hali anuwai kabisa inayoweza kuvutwa gharama kulipiwa.
Maamuzi yaliyoahirisha
Jambo linapohusisha mashindano magumu ya kisheria Mjumbe wa Baraza anaweza kuhitaji kuahirisha uamuzi wao.
Maana yake ni kwamba uamuzi haamuliwi moja kwa moja baada ya hukumu. Badala yake, Mjumbe wa Baraza atachukua muda kukagua ushahidi na legislation (Kupatikana kwa Kiingereza tu) na kuamua uamuzi wao baadaye.
Kawaida maamuzi yaliyoahirisha yanatolewa kwa upande wote kwa muundo wa maandishi na sababu ndani za kueleza jinsi Mjumbe wa Baraza ameamua uamuzi wao.
Sababu za maandishi kwa uamuzi
Chini ya section 49 ya Consumer, Trader and Tenancy Tribunal Act 2001, upande wa utendaji wanaweza kuomba nakala ya maandishi ya sababu za Mjumbe wa Baraza kuamua uamuzi.
Ombi la sababu za maandishi liwekwe ndani ya siku 14 ya kupokea Notice of Order. Maombi yote kwa sababu za maandishi yafanywe kutumia maandishi kwa Msajili.
Kama amri imeamuliwa na ruhusa, kwa mfano wakati wa upatanisho, ndipo sababu za maandishi haziwezi kuombewa.
Kufunua amri ya CTTT
Kawaida amri ya CTTT inapatikana pekee kwa upande unaoshiriki katika mabishano. Hata hivyo, baadhi ya amri ya CTTT inapatikana kwa umma. Hiyo ni pamoja na:
- Amri yote iliyoamuliwa chini ya Home Building Act 1989 ambayo inatolewa kwa Kamishna ya Fair Trading kuwa pamoja na usajili wa umma.
- Amri inayotegemewa na sababu za maandishi inayochapishwa kwa Australasian Legal Information Institute's website www.austlii.edu.au
Get a free copy of Adobe Acrobat Reader so you can access PDF versions of our information.